Miili ya watu wanane tu kati ya watu 50 walikufa katika ajali ya juzi, iliyohusisha basi na lori katika eneo la Changarawe, Mafinga mkoani Iringa, ndiyo iliyotambuliwa mpaka mchana.
Idadi
ya marehemu wa ajali hiyo iliongezeka kutoka 42 waliokufa mapema juzi
hadi 50. Mmoja wa hao walioongezeka aliyekuwa amelazwa katika hospitali
ya mkoa wa Iringa, ametambuliwa kuwa ni Oswald Mwinuka (58).
Wakati
taarifa ya awali kutoka vyanzo mbalimbali ilidai wengi waliokufa katika
ajali hiyo, walikuwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, taarifa
iliyotolewa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, Ramadhani Mungi
inaonesha wanaoendelea kutambuliwa walikuwa wafanyabiashara wa eneo la
Soweto, mjini Mbeya.
Ajali
hiyo ilihusisha lori aina ya Scania namba T 689 APJ mali ya Cipex
Company lililokuwa likiendeshwa na Maka Sebastian (26) ambaye amelazwa
katika hospitali ya mkoa wa Iringa akiendelea na matibabu na basi aina
ya Scania namba T438 CED mali ya kampuni ya Majinja lililokuwa
likiendeshwa na Baraka Gabriel (38) aliyekufa papo hapo juzi.
Wakati lori hilo lilikuwa likielekea barabara ya Mafinga-Mbeya, basi hilo lilikuwa likitoka Mbeya kuelekea jijini Dar es Salaam.
Kamanda
wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, Ramadhani Mungi alisema chanzo cha ajali
hiyo ni ubovu wa barabara katika eneo la ajali na mwendo kasi.
Baada
ya magari hayo kugongana, kontena lililokuwa limepakiwa katika lori
hilo lilifyatuka na kupiga basi hilo, hali iliyosababisha mauti na
majeruhi wengi katika ajali hiyo.
Alisema zoezi la kutambua miili hiyo linaendelea katika hospitali ya mkoa wa Iringa na ile ya wilaya ya Mufindi mjini Mafinga.
Alisema imekuwa ngumu kutaja majina ya watu wote waliokufa kwa kuwa hawajatambuliwa na kuthibitishwa na ndugu zao.
Mganga
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Robert Salim alisema kati ya maiti 27
waliofikishwa hospitalini hapo juzi kutoka Mafinga ni wanane tu
waliotambuliwa na kuchukuliwa na ndugu zao, wengi wao kutoka jijini
Mbeya.
Kamanda
Mungi alitaja miili iliyotambulikuwa kuwa ni Mbezi Deogratius (29),
Editha Ngunangwa (28), Mohamed Juma (32) na Ndenya Sixbert (25) ambao
wote walikuwa wakazi wa Soweto Mbeya.
Wengine ni James Kinyamaguho (30) mkazi wa Morogoro, Said Halfan (35) na Abuu Mangula (35) ambao pia ni wakazi wa Mbeya.
Aliwataja
waliojeruhiwa ambao wamelazwa katika hospitali ya mkoa wa Iringa na ya
wilaya ya Mufindi ya Mafinga kuwa ni Mustafa Ally, Dominic Shauri, Tito
Kyando, Martin Haule, Ipyana Mbamba, Fadhil Kalenga, Mussa Mwasege,
Nehemia Mbuji, Josam Abel, Tumpate Mwakapala, Nico Hamis na Ester
William.
Wengine
ni Peter Mwakanale, Kelvin Mwakaladi, Raphael Nerbot, Maga Sebastian,
Catherine Mwijungu, Lucy Mtanga, Debora Vicent, Ester na mwanaume ambaye
jina lake halijaweza kujulikana kutokana na kuwa na hali mbaya.
Mganga
Mkuu wa Mkoa, Dk Salim alisema hali za majeruhi wanne waliolazwa
hospitali ya rufaa ya Iringa inaendelea vizuri wakati wengine wanne hali
zao sio nzuri na wanatarajia kupewa rufaa kwenda hospitali ya Taifa ya
Muhimbili.
Naye
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Mufindi, Boaz Mnenegwa
alisema hali za majeruhi 13 waliobaki Mafinga zinaendelea vizuri.
Wakati
huo huo, Chama cha Wananchi (CUF) kimetoa salamu za pole na rambirambi
kwa ndugu wa waliopoteza maisha na majeruhi wote wa ajali hiyo.
"Tukio hili ni baya sana na la kusikitisha kwa Watanzania. Si rahisi kuelezea tukio hili bila kulengwa ama kutokwa na machozi," ilisema taarifa hiyo.
Chama
hicho kimeeleza kuwa matukio ya namna hiyo yamekuwa yakijitokeza mara
kwa mara na hakuna hatua za mashiko za kumaliza tatizo hili. "Kwa
ajali hii licha ya uzembe waliofanya madereva, lakini miundombinu ya
eneo la ajali haiko sawa kutokana na mashimo yaliyopo."
Kilieleza
kuwa barabara nyingi za lami Tanzania zimeharibika sana na marekebisho
yake huwa yanaweza yasifanyike ama yakafanyika kidogo kiubabaishaji.
"CUF
tunaitaka serikali kupitia upya mfumo wake wa marekebisho ya barabara
ili kuhakikisha ubovu wa barabara hauchangii kabisa katika kuleta ajali
barabarani. Japo hii si tiba ya ajali za barabarini lakini kwa kiasi
fulani itapunguza," alieleza taarifa hiyo.
Chama
hicho kimeitaka Serikali iwawajibishe viongozi wake wazembe wanaotakiwa
kupambana na ajali hizi, lakini hawatimizi majukumu yao.
Hizi ndio sehemu 12 zinazompa Raha mwanamke wakati wa Tendo, Bonyeza Hapa chini== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA VIDEO CHAFU YA AGNESS MASOGANGE== >